Tuesday, 31 January 2017

Mambo ya mahanjumati

JINSI YA KUTENGENEZA.
Roweka mchele kwa 1 hour kaanga vitunguu mpaka viwe brown, kaanga mbatata mpaka ziwive,weka mafuta kwenye sufuria yakipata moto tia bizari nzima, mdalasini mzima, karafuu na hiliki.kaanga kidogo, kisha weka tungule mpaka ziwive vizuri tia vitunguu ulokaanga nusu, kisha tia garlic na tangawizi pamoja na tomato.
Mdalasini wa unga, bizari nzima ya unga na chumvi kaanga mpaka vikaangike uzuri  halafu weka kitoweo chako, mtindi,carrot pilipilihoho,kisha changanya vizuri weka maji wacha kwenye moto kidogo viwive kidogo visivurugike kisha weka lemon juice, masala ya birian na mbatata ulokaanga,changanya vizuri uweke pembeni  kisha weka maji kwenye moto tia samli,mdalasini,hiliki na chumvi yakichemka tia mchele,upike wali mpaka uwive nusu kisha mwaga maji yote, weka nusu wali kwenye sufuria tia rosti lote kisha tia na vitunguu vilobaki kisha malizia wali ulobaki kisha nyunyiza rangi ya orange kisha funika vizuri weka kwenye oven ukikauka vizuri changanya.sasa unaweza kula.