Wednesday, 1 February 2017

AUDIO FILE

JINSI YA KUANDAA MEAT CAKE

HATUA YA KWANZA

Unga, samli, castad pikipowder, saladi, nyama ya kusaga, mayai, chumvi na maji. 
Unasaga unga wako ukimaliza umachangaya na saladi zako pamoja na kuchemsha mayai yako nabkuayakata vipande kisha unachanganya mayai katika unga wako.



HATUA YA PILI

Baada ya matayarisho hayo unachanganya nyama ya ng'ombe ya kusaga mpaka iwe katika muonekano mzuri


HATUA YA TATU 
Baada ya mchanganyiko huo hatua inayofuata ni uchanganyaji wa maziwa katika chakula chako. sasa chakula chako kitakuwa na mchanganyo wa unga, mayai,saladi na maziwa.



Baada ya kumaliza mchanganyiko huo  sasa tunayarisha chakula chetu kwa kukiweka kwenye oven. Kwa muda wa nusu saa kwa moto mdogo mdogo ili chakula chako kiwive uzuri na kiwe na muonekano mzuri


Sasa tayari chakula chako kuliwa na kitakuwa kinaonekana kwa muonekano mzuriiiii.........






 INFORMATION TECHNOLOGY
  Hii ni taaluma nzuri sana ya kujifunza blog



Tuesday, 31 January 2017

Mambo ya mahanjumati

JINSI YA KUTENGENEZA.
Roweka mchele kwa 1 hour kaanga vitunguu mpaka viwe brown, kaanga mbatata mpaka ziwive,weka mafuta kwenye sufuria yakipata moto tia bizari nzima, mdalasini mzima, karafuu na hiliki.kaanga kidogo, kisha weka tungule mpaka ziwive vizuri tia vitunguu ulokaanga nusu, kisha tia garlic na tangawizi pamoja na tomato.
Mdalasini wa unga, bizari nzima ya unga na chumvi kaanga mpaka vikaangike uzuri  halafu weka kitoweo chako, mtindi,carrot pilipilihoho,kisha changanya vizuri weka maji wacha kwenye moto kidogo viwive kidogo visivurugike kisha weka lemon juice, masala ya birian na mbatata ulokaanga,changanya vizuri uweke pembeni  kisha weka maji kwenye moto tia samli,mdalasini,hiliki na chumvi yakichemka tia mchele,upike wali mpaka uwive nusu kisha mwaga maji yote, weka nusu wali kwenye sufuria tia rosti lote kisha tia na vitunguu vilobaki kisha malizia wali ulobaki kisha nyunyiza rangi ya orange kisha funika vizuri weka kwenye oven ukikauka vizuri changanya.sasa unaweza kula.